MAUA YA VALENTINO 🙄😂 Maua niliyokupa, tafadhali yarudishe, Usije ukayatupa, utazua mishemishe, Ewe wakwangu msupa, bora nikufahamishe, Maua niliyokupa, niliiba kaburini. Kaburi nambari tano, ndipo nilipoyatoa, Rangi yake ya manjano, ni rahisi kutambua, Imeninasa ndoano, mzimu wanisumbua, Maua niliyokupa, yarudishe kaburini. 🙄🙄😂😂😂 © Samson Karani. Chemistry Wizard. Garbage Collector, Marembo Market.